DR. KAMALA AKUTANA NA WAFANYA KAZI WA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Jana waziri mpya aliyeteuliwa katika baraza jipya la mawaziri Dr.Diodorus Kamala alikutana na wafanyakazi wa wizara yake ya afrika mashariki nakuwasihi wampe ushirikiano katika kuijenga wizara hii mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dr. Kamala ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa naibu waziri wa wizara hiyo, amemshukuru mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Jakaya Kikwete kwa imani aliyonayo kwake hatimaye kumteua kushika wadhifa huo nyeti, mh. Kamala alisema atahakikisha maslai ya watanzania yanawekwa mbele katika kuelekea kwenye shirikisho la kisiasa la afrika mashariki.
Mh. Dr Kamala aliwashukuru wafanyakazi wote wa wizara kwa ushirikiano wao walio mpa kipindi akiwa naibu waziri na akawaomba wazidi kumpa ushirikiano katika kipindi hiki ambacho amepewa dhamana ya kuiongoza wizara hii nyeti, amewaomba wafanyakazi waunde team work ili waweze kutimiza malengo yao ya kila siku.
Mkutano huo ulio hudhuliwa na viongozi wote wa wizara wakiongozwa na mwenyekiti wao wa chama cha wafanyakazi tawi la wizara ya afrika mashariki ndg. Maguzu, walimwahidi mh. waziri kumpa ushirikiano wa hari na mali ili kufikia malengo ya wizara. Akitoa shukrani zake kwa niaba ya katibu mkuu, ndg Uled alimwahidi mh. waziri ushirikiano na uchapakazi uliotukuka, vilevile alimpongeza kwa kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo.

No comments:
Post a Comment