11/27/08

Nyakijooga mahari wanapohiji wakatoliki wa jimbo la bukoba

9/11/08

Joy ndani ya uwanja mkuu wa taifa akifatilia mechi ya stars na wacameroon mlima kilimanjaro kama unavoonekana angani
Mr blue atoka ugaibuni
kumbe wanacheka pamoja, ni nchimbi mwenyekiti wa uvccm na hasimu wake nape nahuye mlipua mabomu nape nahuye
Joymertha ishengoma akiwa katika pozi Franky theodiry akiwa katika pozi siku ya birthday yake, hongera franky
Dr, Bishanga, Dr, Eric, na Melline wakitoka nje ya jengo alimoishi Livingstone
Hii ndio nyumba inayo aminika kuwa aliishi David livingstone, nyumba hii iko nje kidogo ya manispaa ya Tabora
Bosi wa mradi wa Engender Health-CHAMPION PROJECT Dr. Eric na Mellanier Yahner wakiingia kwenye nyumba alimoishi David Livingstone nje kidogo ya manispaa ya Tabora hivi karibuni
Dr. bishanga akiwa flamingo mgahawa uliopo uwanja wa ndege wa jk nyerere mala baada ya ndege ya shirika la precision kuchelewa kuruka kuelekea tabora, abiria walikaa uwanjani masaa 9

9/1/08

mtaalam akiwatambulisha wageni siku ya send off ya mdogo wake anchila theodory
Bi anchila theodory siku ya send off yake
mtaalam frank akiwashukuru wageni waliofika kwenye graduu yake
wadau waliowezesha uzinduzi wa miss afrika uk wakimsikiliza mgeni rasmi mh. kamala, kutoka kulia ni, Dr. dastan bishanga, mrs greyson, mkuu wa wilaya ya mabibo mtaalam frank, na enjinia greyson

Dr kamala waziri wa afrika mashariki akizindua mchakato wa miss afrika uk, wengine katika picha ni ssebo msemaji wa kamati, katibu deo rweyunga na mwenyekiti allan karinga

wadau humu ni ndani ya air bus
Mtaalam ndani ya Air bus ndege mpya ya ATC akitoka kwenye utafiti mwanza

8/15/08

Dr. kamala akitoa hotuba yake siku ya graduation ya frank

8/12/08

KAULI YA MWISHO YA MAREHEMU MH. CHACHA WANGWE KWA MWENYEKITI WA CHADEMA MH. FREEMAN MBOWE

KAULI YA MWISHO YA MAREHEMU CHACHA WANGWE KWAMWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWEHII NI TAARIFA YA MHESHIMIWA WANGWE KUHUSU JARIBIO LA MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE KUMVUA WADHIFA WAKE NA UANACHAMA WA CHADEMA ALIYOTARAJIA KUISOMA KWA WATANZANIA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUFIKA DAR ES SALAAM, DHAMIRA AMBAYO ILIKATISHWA NA MAUTI YALIYOTOKANA NA INAYOSEMEKANA KUWA NI AJALI YA KUPANGWA, ENEO LA PANDAMBILI, WILAYA YA KONGWA DODOMA TAREHE 28 JULAI, 2008.
Taarifa hii ilikuwa isomwe Dar es salaam, tarehe 29 Julai, 2008 siku moja kabla ya ajali iliyomuua CHACHA WANGWEUTANGULIZIJumamosi, June 28 mwaka huu wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya CHADEMA walidai kuwa wamesitisha Umakau Mwenyekiti wangu katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma siku hiyo. Kesho yake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. FREEMAN MBOWE akaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutaja sababu za kunisimamisha uongozi.
Inatosha tu kusema kuwa sababu zote alizotoa ni za uzushi kama ile inayodai kuwa mimi navujisha siri za chama kwa viongozi wa CCM bila hata kutaja siri hizo, au kusema nimezitoa lini, wapi, na kwa kiongozi yupi?Kikao hicho kinachosemekana kunisimamisha uongozi, kilikuwa na wajumbe 31 ambao takribani nusu hawakuwa na uhalali wa kupiga kura kinyume cha katiba na kanuni za CHADEMA kwa vile walikuwa wameandaliwa kwa kazi hiyo. Wajumbe 7 walikataa kushiriki njama hizo.
Kufuatia jaribio hilo la kunivua uongozi kutokubalika kwa wanachama walio wengi wa CHADEMA , Mwenyekiti MBOWE na wafuasi wake wameendelea kuhaha kwa kuongeza sababu nyingine mbalimbali ili kuhalalisha njama zao. Sasa hivi wameingia hatua ya kuwashawishi wanachama wa Tarime eti wanifukuze uanachama.Kwa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu za CHADEMA, nilichokifanya mimi baada ya kubaini njama zao ni kukata rufaa kwa Baraza Kuu la Chama, kupinga upotoshaji unaofanywa chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE anayeonekana kutaka kuendesha chama kinyume na matarajio ya wanachama walio wengi.Hivyo basi zipo habari za uhakika kuwa kikao hicho cha Baraza Kuu hakitaitishwa ama kabisa, au kitacheleweshwa kwa makusudi, kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kutokuwa na fedha za kukidhi gharama za kikao hicho.
Naomba nikiri kuwa ninakerwa sana na mtiririko mzima wa sakata hili linalozua mgogoro unaokiyumbisha chama. Ukweli ni kwamba mimi niligombea Umakamu Mwenyekiti nikiwa na agenda ya kufufua uhai wa chama kwa kukaripia vitendo visivyostahili katika kuendesha chama. Agenda yangu haijabadilika. Yote niliyoyasema wakati nagombea nafasi hii yanafahamika kwa wana CHADEMA wote.
Walikuwepo walioyalalamikia na walikuwepo walioyapongeza matamshi yangu hayo.Mwisho wa yote wana CHADEMA waliridhika kuwa ajenda yangu ilikuwa sahihi na hivyo wakanichagua kuwa Makamu Mwenyekiti. Hivyo basi hata kama ni kweli kuwa ulikuwepo mvutano wakati wa kampeni ile, lakini hilo ni jambo la kawaida katika uchaguzi. Nijuavyo mimi hayo yalitakiwa yawe si ndwele nasi tugange yajayo kwani wanachama walikwisha fanya uamuzi halali kupitia kura zao.
Baada ya kuingia kwenye wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Taifa, nilifanikiwa kuzungumza na Mhe. MBOWE kuhusu mambo, hususan yale, niliyoyapigania wakati wa kinyang?anyiro kile na kumuomba tukae chini na kutafuta jinsi ya kufanikisha azma hiyo.Ni imani yangu kuwa waraka huu utawasaidia wanaCHADEMA wenzangu na watanzania wote kwa ujumla, kuelewa vizuri ukweli wa mambo niliyoyapigania kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti, na ninayoendelea kuyasimamia hivi sasa nikiwa Makamu Mwenyekiti, na inshallah nitakayoyatekeleza baadae kama Taifa Mwenyekiti wa CHADEMA.
Kimsingi mambo tunayotofautiana na Mhe. MBOWE ni haya yafuatayo:-MATUMIZI YA RUZUKUCHADEMA hupata ruzuku ya Tshs. 66,000,000 kwa mwezi (Milioni sitini na sita). Mimi nasema si haba hasa tukizingatia chama kilikotoka. Naamini kuwa kiasi hiki cha fedha kikisimamiwa vizuri kinaweza kukirahisishia chama kujieneza katika ngazi zote toka Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.
Si kweli kwamba matatizo yote yatamalizwa na fedha hizi lakini basi hata ofisi za chama zinaweza kuwa hai nchi nzima kitu ambacho kwa sasa hakipo. Mahesabu yanaonesha kuwa mtaji wa laki moja (Tshs.100,000/=) kwa wilaya moja nchini inatosha, hivyo kwa Wilaya 126 kwa mwezi jumla yake ni Tshs. milioni 12 (Tshs. 12,600,000/= ) zinahitajika ( Wilaya 126 x 100,000 kila wilaya = 12,000,000/=)Hata tukisema tupeleke kiasi hicho kwa kila jimbo la uchaguzi jumla yake ni Tshs. Milioni 23 (Tshs. 23,000,000/=) kwa maana ya majimbo 213 x 100,000 = 23,000,000/=.
Mhe. MBOWE anasema hizo ni pesa nyingi sana kwa uimarishaji wa chama. Mimi nasema hapana, kiwango hiki kwa kila Wilaya au Jimbo la uchaguzi ni muafaka kwani haba na haba hujaza kibaba.Chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE na wafuasi wake hawastaajabu kuwa kati ya Tshs. 374,144,000.40 zilizopatikana kama ruzuku katika ya Januari 1 na Juni, 30, 2008, Tshs. 350,000,000/= zilitumika Makao Makuu ya CHADEMA na Tshs. 25,000,000/= tu ndizo zilikwenda Wilayani kuimarisha chama.Mimi naona mgao huu unayatukuza Makao Makuu ya
CHADEMA isivyostahili wakati huo huo ukidhalilisha chama nchi nzima.
MADENI YA UCHAGUZIKufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa na Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa chama kimekwisha mlipa Tshs. 175,000,000/=Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha Wilayani na Makao Makuu niliamua kumshauri MBOWE asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa toka serikalini.
Mhe. MBOWE alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibishie pesa hizo anazodai alikikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya CHADEMA, kupitia hundi ipi, na lini? Nilimuomba pia kutaja ni kikao gani cha chama kiliidhinisha matumizi ya fedha hizo kwani kama hakuna ushahidi wa maidhinisho, ni dhahiri kuwa matumizi hayo hayakudhibitiwa na chama na kwa mantiki hiyo kuyafanya kuwa matumizi binafsi ya Mhe. MBOWE.Vilevile, nilimueleza kuwa matumizi ya fedha hizo alizodai alikikopesha chama yalikuwa yakinuka harufu ya UFISADI.
Stakabadhi zote kuhusiana na matumizi hayo zilionesha kuwa gharama za aidha ununuzi na / au ukodishaji wa vifaa hivyo, hazikutofautiana na viwango wanavyolipishwa watalii kwa huduma kama hizo, kwa maana ya gharama ya juu sana.Na kwa kuwa hata baada ya kuwa Mhe. MBOWE amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya deni alilodai kuikopehsa CHADEMA, vifaa vyote yakiwemo magari, vipaza sauti na kadhalika vimebakia kuwa mali yake binafsi, basi bila kumficha nilimueleza kuwa huko ni kukinyonya chama kwa kukigeuza kitega uchumi cha watu binafsi.Kuhusu suala la kulipa madeni kupitia ruzuku ya serikali, nilimuomba Mhe. MBOWE afuatilie kwa Msajili wa Vyama vya siasa ili tupate ufafanuzi kama kweli fedha za ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa, inaweza kutumika kulipia madeni ya viongozi wa vyama hivyo yatokanayo na uchaguzi ili CHADEMA isiathirike kisheria.
Niseme kweli hapa kwamba, kwa vile wanaCHADEMA wengi walinichagua kuwa Makamu Mwenyekiti, na hata mimi mwenyewe tulikuwa wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani n.k katika uchaguzi wa mwaka 2005 ningefarijika sana iwapo na sisi tungerejeshewa angalau chochote cha kufidia gharama zetu, kwa maana kwamba kama chama kimeamua kurudisha gharama hizo kiwalipe wote badala ya kulipa madeni kwa wateule wachache.UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUMNaamini ukweli wa suala hili hauna mjadala. Kwamba Mhe. MBOWE na wafuasi wake walighushi orodha ya majina ya viti Maalum badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu sio siri.
Naamini hata Mhe. MBOWE anakubaliana nami kuwa suala hili si moja ya siri anazodai nimevujisha! Yamesemwa mengi juu ya mtafaruku uliojitokeza kuhusu viti maalum hadi baadhi ya waasisi wa chama wakataka kujitoa na hivyo kumlazimisha Mwenyekiti Taifa ( FREEMN MBOWE) na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kukiomba radhi kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama katika suala hili la kugushi viti maalum.
Ni ukweli ulio wazi kuwa kitendo hicho cha upendeleo bado kina iumiza taswira ya CHADEMA. Chama kinaonekana kuendekeza ujanja ujanja kiasi kwamba watu na binti zao, wakwe zao, shemeji zao, waume wenzao, wachumba wa shemeji zao, wake wenza na kwa kiwango kikubwa watu wa kabila moja ndiyo wamekuwa sura ya CHADEMA bungeni.Katika hili nilichoweza kumueleza Mhe. MBOWE ni kuwa chaguzi mbalimbali tangu za Mitaa, Ubunge na Urais zinakaribia ni vizuri tufanye bidii kusambaza nguvu zetu nchi nzima tuwe na mtaji wa kura maeneo mengi ili kashfa kama hii isijirudie. Hii ni kwa msingi kuwa chama kikijitanua kutakuwa hakuna sababu ya kuwaona watu wa eneo fulani tu kuwa ndiyo mhimili wa CHADEMA na hivyo zikitokea fursa itakuwa rahisi chama kuwakilishwa na mtandao wake mpana badala ya koo au kabila fulani.Sasa kwa kuwa kuimarisha chama kitaifa maana yake ni matumizi ya fedha, nalo hili likawa nongwa ingawa kwa mtazamo wa Makao Makuu kulipa madeni kwa wateule wachache si nongwa.
Cha ajabu ni kwamba Mhe. MBOWE hakukana kuwa hili la viti maalum na hata upangaji wa ajira kwa ukabila una leta athari mbaya kwa mustakabali wa CHADEMA.Katika maongezi yangu nae nilikuwa wazi nilipotahadharisha kuwa:
1. Watanzania wakiendelea kuona kwamba CHADEMA inaendeshwa kwa misingi ya kikabila hawatajiunga na chama chetu na tutakosa wafuasi.
2. Watanzania wakiona kuwa sisi tumeweka mbele ukabila kuliko utaifa hawatatupa madaraka na kutawala kwa kuhofia yale yanayotokea nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Kenya na kadhalika ambako nafasi za raia wote zimehodhiwa na kabila moja na hatma yake watu wamechinjana kama kuku kwa kupinga hilo.
Pia nilimwambia kwamba, kwa jinsi sura ya uteuzi wa Wakurugenzi na watendaji wengine wa Makao Makuu inavyoonekana, sasa tayari chama chetu kimebatizwa jina la CHAMA CHA WACHAGA, na hii si kuwatendea haki raia wengine na makabila yao ambao wataonekana kama punguani kujihusisha na chama na ukabila.Yote haya ninayosema kuhusu ukabila, upendeleo na kadhalika sio dhana tu. Kufuatia malalamiko mengi yaliyokuwa yakisikika nchi nzima kuhusu masuala haya, Kamati Kuu ya CHADEMA ilikwisha unda Tume kutafuta ukweli wa mambo hayo. Tume hiyo ya watu watano iliongozwa na Mhe. Merky Lugendo Mziray ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA nayo imekwisha toa taarifa yake kwamba Makao Makuu ya CHADEMA yanatawaliwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kielimu.
UTENDAJI WA KIBABECHADEMA ni chama kilicho njia panda kwa sasa kutokana na utendaji wa kibabe wa Mhe. MBOWE. Ninafahamu jinsi vyama vingine vya upinzani hapa nchini kama vile NCCR ? Mageuzi vilivyoporomoka haraka haraka mithili ya nyumba ya mabua. Chama NCCR ? Mageuzi kilifikia mahali pazuri tu hadi watu wakaanza kufikiria kuwa kingekuwa chama mbadala kwa CCM.
kwa bahati mbaya uchu wa madaraka, ulafi wa ruzuku, na tabia za kimangimeza kwa pamoja vikakiathiri hadi kupoteza umaarufu wake.Na hata vyama vingine vya upinzani vina dalili hizo hizo japo kwa viwango vinavyotofautiana. Ila badala ya kujichunguza na kujua kasoro zetu, kila siku vyama vyetu, vimekuwa vikidai kuwa ni chama tawala ndicho kinachoviroga, kama ambavyo Mhe. MBOWE ameanza kuweweseka kupitia vyombo vya habari.Napenda kuthibitisha kuwa katika mgogoro unaopaliliwa sasa na Mhe. MBOWE ndani ya CHADEMA kutokana na ufisadi, ufuska, ulevi wa madaraka na umangimeza chanzo chake ni tabia yake ya kuendesha chama kibabe. Mathalan kumzuia Martin Mung?ong?o Mkurugenzi aliyechaguliwa kwa kura kutofanya kazi zake ndani ya chama, madai ya kupigana na watendaji wa chama ndani ya baa na vitendo vingine vya aina hiyo ni ushahidi tosha wa hulka hii.
Hadi sasa Mhe. MBOWE amefanikiwa kukizuia chama hiki kisifanye kazi ya siasa mkoa wa Dar es salaam kwa miaka minne.Ninavyoongea hivi sasa CHADEMA imekuwa ikikimbia vikao vya Democratic Union of Afrika (DUA), Muungano wa Vyama Vya Upinzani, uliofanikisha CHADEMA kujuana na Conservative Party ya Uingereza na Republican ya Marekani. Vyama dada hivi vyote vinaulalamikia uongozi wa CHADEMA kwa kufuja fedha ya misaada na kuwasilisha kwao risiti za kugushi, kama ilivyofanyiwa Conservative Party baada ya kutoa msaada wa Tshs. 78,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli na pikipiki ambazo hazikununuliwa.Katika mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA huko Dodoma hivi majuzi tu, Mhe. MBOWE kwa kauli yake aliwatisha wajumbe kuwa alikuwa amethibiti uwezekano wowote wa wajumbe kujisikia huru kwa kutoa mawazo ambayo yangepingana na ajenda yake aliyoitoa ghafla kikaoni kunisimamisha Umakamu Mwenyekiti.
Mhe. MBOWE Alikifahamisha kikao kuwa alitoa taarifa kwa IGP, SAID MWEMA kuwa kuna wahuni ambao walitaka kuuchafua mkutano wake, naye IGP akahakikisha kuwa mkutano ule unalindwa kwa kiwango cha kushtua kama ambavyo hata vyombo vya habari vimethibitisha.Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayobainisha Mhe. MBOWE ni kiongozi wa aina gani.
HITIMISHOKama nilivyokwisha sema hapo awali, sijaacha na sintoacha ajenda yangu ya kufufua uhai wa CHADEMA kwani ndiyo ahadi iliyofanikisha kuchaguliwa kwangu kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa. Nilipopata wadhifa huo nilianza kuitekeleza ajenda hiyo kupitia mahojiano na Mwenyekiti MBOWE kuhusu matumizi ya ruzuku, madeni ya uchaguzi, uteuzi wa wabunge wa viti maalum, nafasi za ajira Makao Makuu, na kuhusu mwenendo wa chama Mkoa wa Dar es salaam.
Nilijikuta katika mvutano mkubwa kila nilipogusa eneo lolote katika haya. Nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa sikuwa na uwezo wa kubadili mambo hayo yaliyokuwa yakiratibiwa kwa ukaribu na Mhe. MBOWE na wafuasi wake kwani sikupewa ushirikiano wa aina yoyote na chama pale Makao Makuu.
Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu, sikupewa vitendea kazi kama magari, vipaza sauti na/au vyombo vya habari, na sikuwahi kupata taarifa yoyote ya kiutendaji toka Makao Makuu.Kwa kuzingatia yote hayo, naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati wanachama wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam ambao kwa pamoja tulisimama kidete kufufua uhai wa chama hapa jijini. Niseme tu ushirikiano wao wa hali na mali uliniwezesha kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa.
Rai yangu kwa wana CHADEMA na wale wote wanaokitakia mema chama chetu na nchi yetu kwa ujumla ni kwamba kazi ya kupigania demokrasia ya kweli ndani na nje ya chama, kukiepusha chama na vitendo vya ukabila, migogoro, ubadhirifu, umangimeza, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote bado inaendelea na nawaombeni mniunge mkono kwa hali na mali katika vita hii. Naamini tutashinda.Mungu Ibariki CHADEMAMungu Ibariki TanzaniaMungu Ibariki Afrika….Chacha Wangwe amekufa lakini waraka wake huu utawasaidia WanaCHADEMA na watanzania kuelewa ukweli wa mambo aliyokusudia.

7/10/08

Mtaalam mpiganaji franky akiwa ndani ya johoo mara baada ya kutunukiwa degree yake ya mambo ya mazingira
wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wakiomba dua kabla ya kuanza kikao cha leo asubui, bunge la sasa ni moto kwelikweli lina washughulikia mafisadi haswa
Spika wa bunge la muungano mh samwel sitta mzee wa speed na viwango

Mh LUHAGA MPINA mmoja wa wabunge vijana machachari ambao wanasimamia hoja za msingi zinazowahusu watanzania walio na mzigo mzito wa umaskini, mh. MPINA kazihilisha hilo wakati anachangia hoja ya waziri wa nishati na madini jana bungeni. Mh MPINA alisema "mh spika nashukuru kwa kunipa nafasi hii, kwanza kabisa mimi siihungi mkono hoja hii, na ntarudi kwenye kanuni za bunge" hapa anazisoma kanuni" wakati wa mafungu ntaondoa shilingi yangu kwenye mshahala wa waziri" spika ana mkatiza..... badae anaendelea"mpaka hapo ntakapopata ufafanunuzi wa kutosha kuhusu wapiga kura wangu"anavitaja vijiji"mh. spika namuomba mh waziri anipe majibu nijirizishe. Wabunge kama mh. MPINA ni wachache sana katika bunge letu tukufu, niwabunge ambao hata wakifa roho zao zinabaki hai, sio wakifa wanakufa completely. Aksante sana mh. vijana tunataka wabunge kama wewe, sendeka, kimaro, kilango nawengine wengi wanao tetea maslai ya wananchi,huu ni uthibitisho tosha kuwa wapiga kura wako wa jimbo la kisesa hawakukosea kukupa kura na hatimaye ukapata ushindi wa kishindo.

6/27/08

MH. DR KAMALA waziri wa afrika mashariki na mbunge wa jimbo la nkenge na wife wake mama ketty walikuwepo kwenye hafla ya kumpongeza mtaalam frank kwa kuweza kuhitimu degree yake
Hapa mtaalam frank akimlisha mama yake THEONESTINA RWECHUNGURA KEKI, kushoto kwa mama ni rafiki yake frank, richard, kulia kwa mama ni afred na uncle wake frank mwalimu JOSEPH.
Naam wadau huyu ndiye mwenyewe haswa mtaalam FRANK THEODORY hapa ni baada ya kutunukiwa degree yake ya kwanza ya mambo ya geografia na mazingira. Hongera sana MTAALAM.
Mama ajuna "MRS MUSHUMBUSI" akiwa na ajuna siku ya birthday ya aunt yangu AJUNA