7/10/08

Mtaalam mpiganaji franky akiwa ndani ya johoo mara baada ya kutunukiwa degree yake ya mambo ya mazingira
wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wakiomba dua kabla ya kuanza kikao cha leo asubui, bunge la sasa ni moto kwelikweli lina washughulikia mafisadi haswa
Spika wa bunge la muungano mh samwel sitta mzee wa speed na viwango

Mh LUHAGA MPINA mmoja wa wabunge vijana machachari ambao wanasimamia hoja za msingi zinazowahusu watanzania walio na mzigo mzito wa umaskini, mh. MPINA kazihilisha hilo wakati anachangia hoja ya waziri wa nishati na madini jana bungeni. Mh MPINA alisema "mh spika nashukuru kwa kunipa nafasi hii, kwanza kabisa mimi siihungi mkono hoja hii, na ntarudi kwenye kanuni za bunge" hapa anazisoma kanuni" wakati wa mafungu ntaondoa shilingi yangu kwenye mshahala wa waziri" spika ana mkatiza..... badae anaendelea"mpaka hapo ntakapopata ufafanunuzi wa kutosha kuhusu wapiga kura wangu"anavitaja vijiji"mh. spika namuomba mh waziri anipe majibu nijirizishe. Wabunge kama mh. MPINA ni wachache sana katika bunge letu tukufu, niwabunge ambao hata wakifa roho zao zinabaki hai, sio wakifa wanakufa completely. Aksante sana mh. vijana tunataka wabunge kama wewe, sendeka, kimaro, kilango nawengine wengi wanao tetea maslai ya wananchi,huu ni uthibitisho tosha kuwa wapiga kura wako wa jimbo la kisesa hawakukosea kukupa kura na hatimaye ukapata ushindi wa kishindo.